﻿Zaburi.
134.
Wimbo wa kwenda juu. Msifuni Mwenyezi Mungu, ninyi nyote watumishi wa Mwenyezi Mungu, ninyi mnaotumika usiku ndani ya nyumba ya Mwenyezi Mungu. 
Inueni mikono yenu katika patakatifu na kumsifu Mwenyezi Mungu. 
Naye Mwenyezi Mungu, Muumba wa mbingu na dunia, awabariki kutoka Sayuni. 
