﻿Zaburi.
133.
Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza ndugu wanapoishi pamoja katika umoja! 
Ni kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa kichwani, yakitiririka kwenye ndevu, yakitiririka kwenye ndevu za Haruni, hadi kwenye upindo wa mavazi yake. 
Ni kama umande wa Hermoni ukianguka juu ya Mlima Sayuni. Kwa maana huko ndiko Mwenyezi Mungu alikoamuru baraka yake, naam, uzima hata milele. 
