﻿Zaburi.
131.
Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. Moyo wangu hauna kiburi, Ee Mwenyezi Mungu, macho yangu hayajivuni; sijishughulishi na mambo makuu kunizidi wala mambo ya ajabu mno kwangu. 
Lakini nimetuliza na kunyamazisha nafsi yangu; kama mtoto aliyeachishwa kunyonya na mama yake, kama mtoto aliyeachishwa kunyonya ndivyo ilivyo nafsi iliyo ndani yangu. 
Ee Israeli, mtumaini Mwenyezi Mungu tangu sasa na hata milele. 
