﻿Zaburi.
129.
Wimbo wa kwenda juu. Wamenitesa sana tangu ujana wangu; Israeli na aseme sasa: 
wamenitesa sana tangu ujana wangu, lakini bado hawajanishinda. 
Wakulima wamelima mgongo wangu, na kufanya mifereji yao mirefu. 
Lakini Mwenyezi Mungu ni mwenye haki; amenifungua toka kamba za waovu. 
Wale wote wanaoichukia Sayuni na warudishwe nyuma kwa aibu. 
Wawe kama majani juu ya paa, ambayo hunyauka kabla hayajakua; 
kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake, wala akusanyaye kujaza mikono yake. 
Wale wapitao karibu na wasiseme, “Baraka ya Mwenyezi Mungu iwe juu yako; tunakubariki katika jina la Mwenyezi Mungu.” 
