﻿Zaburi.
128.
Wimbo wa kwenda juu. Heri wale wote wamchao Mwenyezi Mungu, wanaoenda katika njia zake. 
Utakula matunda ya kazi yako; baraka na mafanikio vitakuwa vyako. 
Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao ndani ya nyumba yako; wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni kuizunguka meza yako. 
Hivyo ndivyo atakavyobarikiwa mtu amchaye Mwenyezi Mungu. 
Mwenyezi Mungu na akubariki kutoka Sayuni siku zote za maisha yako, na uone mafanikio ya Yerusalemu, 
nawe ujaliwe kuishi uone watoto wa watoto wako. Amani iwe juu ya Israeli. 
