﻿Zaburi.
117.
Msifuni Mwenyezi Mungu, enyi mataifa yote; mtukuzeni yeye, enyi watu wote. 
Kwa kuwa upendo wake kwetu ni mkuu, uaminifu wa Mwenyezi Mungu unadumu milele. Msifuni Mwenyezi Mungu. 
