﻿Zaburi.
93.
Mwenyezi Mungu anatawala, amejivika utukufu; Mwenyezi Mungu amejivika utukufu tena amejivika nguvu. Dunia imewekwa imara, haitaondoshwa. 
Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani; wewe umekuwa tangu milele. 
Bahari zimepaza, Ee Mwenyezi Mungu, bahari zimepaza sauti zake; bahari zimepaza sauti za mawimbi yake. 
Yeye ni mkuu kuliko ngurumo ya maji makuu, ni mkuu kuliko mawimbi ya bahari: Mwenyezi Mungu aishiye juu sana ni mkuu. 
Ee Mwenyezi Mungu, sheria zako ni imara; utakatifu umepamba nyumba yako pasipo mwisho. 
